Muswada wa kuruhusu bastola bila leseni Texas

 


Muswada ambao unaruhusu ubebaji wa bastola bila ya leseni, ulipitishwa kwa kura nyingi katika Baraza la Wawakilishi la jimbo la Texas nchin Marekani (USA).


Baraza la Wawakilishi la Texas lilituma muswada huo kwa Seneti, ili kuruhusu ubebaji wa bastola bila kuhitaji leseni au mafunzo ya kulenga risasi, na "kukubalika" kwa kura 84 dhidi ya kura 56 za "kukataliwa".


Inafahamika kuwa Texas, ambapo kuna zaidi ya wamiliki milioni 1.6 wa bastola wenye leseni linaweza kuwa jimbo lenye idadi kubwa zaidi ya wabebaji bastola bila leseni ikiwa muswada huo utapitishwa kuwa sheria.


Wanachama wa Kidemokrasia wa Baraza la Wawakilishi wanapinga muswada huo ambao unarahisisha ubebaji silaha kwa madai kwamba inaweza kuongeza vurugu za mashambulizi.


Muswada huo utaanza kutumika rasmi ikiwa utapitishwa na Seneti.

Post a Comment

0 Comments