Shamsa Ford ampa onyo kali Shilole "Msiruhusu watu kuwa washauri wa ndoa yenu ikitokea shida yamalizeni ndani"


Baada ya kufunga ndoa Shilole na mume wake Romy ameibuka msanii wa bongo movie Shamsa Ford na kuwapongeza kwa kufunga ndoa na akiwapa onyo kali pindi ikitokea wamegombana basi wayamalize ndani bila kuomba ushauri kwa mtu.

Shamsa ford  ametoa kauli hui kupitia ukurasa wake wa instagram huku akidai kuwa naye atanatamani kuolewa.

 "Mashaallah Mashaallah wifi yangu hongera sana .Kwa jinsi ninavyomjua kaka yangu huyu hakika mtafika mbali .Neno SAMAHANI na NIMEKUSAMEHE iwe nguzo ya ndoa yenu .Msiruhusu watu kuwa washauri wa ndoa yenu nyie ni watu wazima kwenye shida yamalizeni wenyewe si kuwapa watu faida.Inshallah ikawe kheri my wiii .Nimetamani sijui na mm niolewe 🙈🤔

@officialshilole @rommy3d hongereni sana"

Post a Comment

0 Comments