Apr 19, 2021

Tetesi za soka kimataifa

  Muungwana Blog 3       Apr 19, 2021


 Barcelona bado haijampatia ofa mpya Lionel Messi,33, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Uhispania unakamilika msimu huu wa joto. (Marca)

Mazungumzo kati ya mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele kuhusu mkataba mpya yanaendelea, huku mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23-ukitarajiwa kumalizika mwaka 2022. (Sport - in Spanish)

Kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino ana matumaini mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe,22, atakubali kufikia mkataba mpya na klabu hiyo. (Goal)

Alexandre Lacazette amesema uamuzi kuhusu mkataba mpya Arsenal "sio wangu pekee", wakati mkataba wa sasa wa mshambuliaji huyo wa Ufaransa aliye na umri wa miaka 29- ukitarajiwa kukamilika mwaka 2022. (Mirror)

Wazo la mshambuliaji wa Italia Moise Kean, 21, kurejea Everton bade ya kuwa PSG kwanza mkopo ni "ngumu kufikiria", kwa mujibu wa ndugu yake Giovanni. (Tuttosport, via Football Italia)

Kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann amekariri kuwa hajafanya mazungumzo na Bayern Munich juu ya kumbadilisha Hansi Flick kama kocha wao. (Goal)

Inter Milan wanataka kumsaini mchezaji Emerson Palmieri,26, kutoka Chelsea. (Todofichajes - in Spanish)

Mchezaji wa kimataifa wa Poland na mlinda mlango wa zamani wa Arsenal Wojciech Szczesny, 31, hataondoka Juventus kujiunga na Tottenham msimu huu. (Goal)

Mkurugenzi wa AC Milan Ricky Massara anasema kuwa anatarajia klabu hiyo itafikia mkataba mpya na mshambuliaji wa Kiswidi Zlatan Ibrahimovic, 39, na ana "imani" mlinda mlango wa Italia Gianluigi Donnarumma, 22, na kiungo wa kati wa Uturuki Hakan Calhanoglu, 27, watatia saini mkataba mpya katika klabu hiyo ya Serie A. (DAZN, via Football Italia)

logoblog

Thanks for reading Tetesi za soka kimataifa

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment