Apr 22, 2021

Wanaosema mitandaoni kuwa Hayati Magufuli alipewa sumu, waaache kuleta uchonganishi- Rais Samia

 


“Kila Mtu Duniani atapata umauti na kila mauti ina sababu, nimeona kwenye Mitandao taaarifa za uchonganishi, taaarifa tuliyopewa na Madaktari ya kifo cha Hayati Magufuli ni tatizo la Moyo, nimekua naona mitandaoni wanasema fulani na fulani wamempa sumu, waaache hili” Rais SAMIA

“Wanaosema mitandaoni kuwa Hayati Magufuli alipewa sumu, mara fulani na fulani walitega kitu, kama wana taarifa za maana waje tuwasikilize, lasivyo waache kuleta uchonganishi, kama wanafanya hivyo kwasababu hatutowapata warudi kwa Mungu wajiulize je wanafanya sawa!?” Rais SAMIA

“Wanaoleta uchonganishi kwenye Mitandao nadhani wanafanya hivyo kwasababu wanajua hatutoweza kuwapata, wanatumia mifumo hiyo huko mingine ambayo bado hatujawa na uwezo wa kuwatafuta, lakini niwaambie tutawatafuta" Rais SAMIA

“Taarifa zinazotolewa mtandaoni (kuwa Hayati Magufuli alipewa sumu), ni za kugonganisha Koo na Koo, Makabila na Makabila, wanaochanganisha kama wanajizatiti wanafanya hivyo kwasababu hatutowapata warudi kwa Mungu wajiulize je wanayofanya ni halali?, wao wangekubali?” Rais SAMIA

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger