Wanasayansi wagundua maiti ya kale ya mwanamke mjamzito Misri


Timu ya wanasayansi nchini Poland imesema wamegundua maiti pekee ya kale ya mwanamke mjamzito huko Misri iliyokuwa imehifadhiwa.

Ugunduzi huo umebainika na wanasayansi wa eneo la hifadhi ya maiti la Warsaw na kuandikwa katika jarida la Sayansi la Akiolojia.

Hifadhi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2015, na inatumia teknolojia ya kisasa kutathmini viti vya kale vilivyohifadhiwa katika Makubusho ya Taifa iliyopo Warsaw.

Awali, maiti hiyo ilikuwa ikidhaniwa kuwa ya kasisi wa kiume lakini uchunguzi wa CT Scan ukaonesha kuwa ni maiti ya mwanamke aliyekuwa hatua ya mwisho ya ujauzito.

Wataalam kutoka hifadhi hiyo wanaamini kuwa mabaki hayo yalikuwa ya mwanamke wa hadhi ya juu kati umri wa miaka 20 na 30, aliyefariki dunia karne ya kwanza kabla ya kristo.

"Kinachooneshwa hapa ndio mfano pekee unaojulikana wa maiti ya kale ya mwanamke mjamzito," makala katika jarida hilo imeandikwa ikitangaza utafiti wake.

Kwa kutumia urefu wa kichwa cha mtoto aliyekuwa tumboni, walikadiria alikuwa kati ya wiki 26 na 30 wakati mama yake anafariki dunia kwasababu ambazo hazikufahamika.

"Ni muhimu sana kufikia utafiti huu, unashangaza kweli," mmoja wa timu hiyo Wojciech Ejsmond kutoka chuo cha Sayansi cha Uholanzi amezungumza na Shirika la Associated Press.

Wanasayansi walisema haikufahamika kwanini mtoto huyo hakuwa ametolewa tumboni lakini kilichoshukiwa kuchangia hilo ni imani juu ya maisha baada ya kifo au pengine kulikuwa na changamoto ya kufanya hivyo.

Post a Comment

0 Comments