Afrika Kusini yapokea dozi ya kwanza ya Pfizer

Jamhuri ya Afrika Kusini imepokea sehemu ya kwanza ya chanjo ya Pfizer ya Ujerumani iliyotengenezwa dhidi ya virusi vya corona.

Waziri wa Afya Zweli Mkhize alirusha picha ya chanjo zilizopakuliwa kutoka ndege za mizigo katika Uwanja wa Ndege wa OR Tambo kwenye akaunti yake ya Twitter.

Nchi itapokea dozi milioni 4.5 za chanjo ya Pfizer mwishoni mwa Juni.

Afrika Kusini iliacha kutumia chanjo ya Uingereza ya AstraZeneca kwa sababu haikuwa na ufanisi dhidi ya mabadiliko ya virusi na kuanza kutumia chanjo za Marekani ya  Johnson & Johnson.

 

Post a Comment

0 Comments