May 4, 2021

Breaking News: Majina ya waamuzi wa mchezo kati ya Simba v Yanga yawekwa hadharani

 


Kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba v Yanga, Mei 8, Shirikisho la Soka Tanzania,  (TFF) limetoa orodha ya waamuzi watakaosimamia mchezo huo.

Huu unakuwa ni mchezo wa pili kwa watani hawa kukutana ambapo ule wa awali walipokutana Uwanja wa Mkapa, Novemba 7 ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imemtaja Emmanuel Mwandembwa kutoka Arusha kuwa mwamuzi wa kati.

Frank Komba wa Dar kuwa mwamuzi msaidizi namba moja.

Hamdan Said kutoka Mtwara kuwa mwamuzi msaidizi namba mbili.

Na Ramadhan Kayoko kutoka Dar kuwa mwamuzi wa akiba.KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger