https://monetag.com/?ref_id=TTIb Breaking: Yanga yapinga mabadiriko ya muda, kuingiza wachezaji saa 11 | Muungwana BLOG

Breaking: Yanga yapinga mabadiriko ya muda, kuingiza wachezaji saa 11

 


Uongozi wa Klabu ya Yanga umeeleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya mabadiliko ya muda wa Mchezo baina ya Simba SC na Yanga SC yaliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoka saa 11:00 jioni hadi saa 1:00 usiku.

Taarifa iliyotolewa na @yangasc imeeleza kuwa Mabadiliko hayo ni kinyume na kanuni ya 15 (10) za Ligi Kuu inayohusu taratibu za mchezo ambayo inasema "Mabadillko yoyote ya muda wa kuanza mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote husika za mchezo angalau saa 24 kabla ya muda wa awali."

Uongozi wa Yanga Umepinga mabadiliko hayo na Kusema kuwa Yanga itapeleka Timu Uwanjani kwa muda wa awali wa saa 11:00 jioni.

Aidha Uongozi wa Yanga umeitaka Bodi ya Ligi na TFF kuendesha Ligi kwa kuzingatia na kuheshimu kanuni zilizowekwa.


Post a Comment

0 Comments