Bunge la Uganda laidhinisha sheria kuhusu uhalifu wa kijinsia

Bunge la Uganda limepitisha sheria ya kina kuhusu uhalifu wa kijinsia, ikifuta baadhi ya vifungu katika sheria ya jinai ya miongo kadhaa.

Hatua hiyo mpya inatoa nafasi ya kubuniwa kwa sajili ya kitaifa ya wahalifu wa kingono.

Mtu yeyote atakayefungwa kwa kuwa mhalifu wa kingono jinalake litaorodheshwa katika sajili hiyo ndani ya siku kumi ya mahakama kutoa hukumu yake.

Watalazimika kutoa maelezo kuhusu historia yao wakati wa kuomba nafasi ya kazi, au nafasi yoyote ambayo inawaweka hatarini watoto wanaowatunza.

Na kwa mara ya kwanza, sheria juu ya unyanyasaji mitaani, unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya umma na vile vile unyanyasaji katika mazingira ya kitaalam imeanzishwa.

Sheria hiyo pia inatoa adhabu ya kifungo cha miaka saba gerezani kwa mtu yeyote atakayesambaza video zilizo na maudhui ya kiutuuzima katika mitandao ya kijamii.

Wanaharakati wanasema sheria hiyo itasaidia kukabiliana na visa vya watu kuvujisha video za ngono kama hatua ya kumhujumu muathiriwa, katika baadhi ya visa video kama hizo zinasambazwa kutoka kwa akaunti ya muathirika.


 

Post a Comment

0 Comments