Chelsea yaishikisha adabu Real Madrid, Yatinga fainali ya UEFA Champions League

UWANJA wa Stamford Bridge, usiku wa kuamkia leo, Chelsea inayonolewa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel imefungua njia na kutinga hatua ya fainali ya UEFA Champions League. 

Mabao 2-0 dhidi ya Real Madrid yanawafanya watinge fainali kwa jumla ya mabao 3-1 mbele ya Kocha Mkuu wa Real Madrid, Zinedine Zidane ambaye alikwama kuibuka na ushindi.

Ni Timo Werner alifunga bao la ufunguzi dakika ya 28 na Mason Mount alipachika bao la pili dakika ya 85 huku lango la Chelsea likiwa katika mikono salama ya Eduardo Mendy.

Ushindi huo unaipa tiketi Chelsea kukutana na Manchester City inayonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola katika fainali inayotarajiwa kuchezwa Mei 29.

Kabla ya kucheza fainali ya UEFA itaanza kazi ya kusaka taji la FA Mei 19 mbele ya Leicester City, Uwanja wa Wembley.

 

Post a Comment

0 Comments