EU yafuta mpango wa kutuma waangalizi wa uchaguzi wa Ethiopia

 


Umoja wa Ulaya EU, umefuta mpango wa kuwatuma waangalizi wake katika uchaguzi wa Ethiopia utakaofanyika mwezi Juni kwa "kutoafikiana kuhusu masuala kadhaa muhimu".

Mwakilishi Mkuu wa Muungano huo Josep Borrell amesema viwango vinavyohitajika kama vile uhuru wa waangalizi na kuingiza nchini humo vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya usalama wao umezuiliwa.

"Inasikitisha kwamba EU haujapewa hakikisho kuhusu kwamba watu wa Ethiopia watapata nafasi ya kushiriki uchaguzi huo kwa njia ya kidemokrasia," aliandika katika taarifa iliyowekwa mtandaoni.

EU imetoa wito kwa serikali ya Ethiopia kuendesha uchaguzi huru na wa haki.

Muungano huo umesema utaunga mkono kwa bodi ya uchaguzi kwa euro milioni 20 ($24m; £17m).

Ethiopia inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu Juni 5. Uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na janga la corona.

Jimbo la Tigray lilipuuza hatua ya serikali na kufanya uchaguzi wake.

Post a Comment

0 Comments