Faida za matumizi ya mbolea za mboji katika kilimo

Matumizi ya mbolea ya mboji katika kilimo cha mazao yana faida zifuatazo;

  • Utengenezaji wa mbolea ya mboji hauna gharama na ni rahisi hivyo wakulima wa ngazi zote wanaweza kuumudu.
  • Mbolea ya mboji huboresha muundo wa udongo unaopelekea kuwa na mzunguko mzuri wa hewa na maji katika udongo.
  • Mbolea ya mboji huongeza virutubisho vinavyohitajika na mmea katika udongo na hivyo kuongeza mazao.
  • Mboji huongeza uwezo wa udongo kutunza maji na hivyo kupunguza kasi ya ukaukaji wa udongo hasa katika maeneo yenye hali ya joto na yasiyopata mvua za kutosha.
  • Mbolea ya mboji huweza kutumika kama mbadala wa mbolea ya samadi wakati wakuandaa kitalu cha mboga.
  • Mbolea ya mboji huboresha afya ya mmea na kufanya uwe na uwezo wa kustahimili magonjwa.

Post a Comment

0 Comments