Kamati ya LAAC yabaini madudu kituo cha Afya Mlali

Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali (LAAC) imetilia mashaka matumizi ya fedha katika ujenzi wa kituo cha afya cha Mlali kilichopo Kata ya Mlali, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro ambapo takribani shilishingi milioni 200 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo zikitumika na kushindwa kukamilisha majengo mawili ya mama na mtoto pamoja na jengo la upasuaji.

Wakizungumza wakiwa katika kituo cha Afya cha Kata ya Mlali wajumbe wa kamati hiyo akiwemo Mheshimiwa Ally Kasinge Mbunge wa Kilwa Kusini na Mheshimiwa Twaha Mpembwenwe Mbunge wa Kibiti wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo wameitaka Halmashauri ya Mvomero kuweka kipaombele katika kituo hicho cha afya ambao kitawasidia wakazi wa Mlali na maeneo jilani na kata hiyo.

“Tunachokiona hapa ni kwamba Halmashauri haijaweka kipaombele katika kituo hiki kwa sababu hata usimamizi wake waulidhishi kabisa.Hata hawa mafundi wamekuja leo baada ya kusikia kuna kamati inakuja hapa watakaa siku mbili tatu wataondoka.”Walisema baadhi ya wajumbe akiwemo Mheshimiwa Twaha Mpembwenwe Mbunge wa Kibiti.

Kufuatia hali hiyo Makamu mwenyekiti wa kamati ya Bunge hesabu za Serikali za mitaa Mheshimiwa Selemani Zedi amewataka watendaji wa Serikali kushirikiana katika kusimamia miradi ya maendeleo, huku Mwenyekiti wa kamati hiyo Grece Tendega akitoa maelekezo ya kukamilika kwa kituo hicho ili kuwaondolea adha ya kutembea ubali mrefu wananchi wa kata ya Mlali na maeneo ya karibu.

“Mkurugenzi huwezi kutoa sababu kuwa umekabidhiwa ofisi miezi ya hivi karibuni hivyo hujui yaliokuwa yakiendelea nyuma, hiyo sio sababu kwa kuwa kuna watendaji uliwakuta lakini pia kuna makabidhiano ya ofisi unapaswa kujua kila kitu kwasababu wewe ndio mkurugenzi kwa sasa na majibu unayoyatoa yanatoka katika ofisi yako”.Alisema Mheshimiwa Selemani Zedi Makamu mwenyekiti wa kamati ya Bunge hesabu za Serikali za mitaa

Kwa upande wao Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mvomero Bw, Hassan Njama na mhandisi wa Wilaya hiyo Silva Mkonda wamesema wamepokea maagizo yote yaliotolewa na kamati,huku wakiahidi kumaliza ujenzi wa kituo hicho cha afya ifikapo mwezi wa saba 2021.

 

Post a Comment

0 Comments