May 4, 2021

Mawaziri wa G7 kujadili haki za binaadamu

  Muungwana Blog 2       May 4, 2021

 


Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi saba zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani, G7 watajadiliana kuhusu haki za binadamu na kitisho cha demokrasia katika siku ya pili ya mkutano wao maalum unaofanyika London, Uingereza. 

Wawakilishi wa Marekani, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Umoja wa Ulaya wanatarajia kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Dominic Raab. 

Ajenda katika mazungumzo ya leo ni pamoja na hali nchini Myanmar, Ethiopia, Somalia, ukanda wa Sahel, Urusi na nchi za magharibi ya ukanda wa Balkan. 

Baada ya mazungumzo hayo, mawaziri hao watakuwa na chakula cha jioni na nchi zilizoalikwa za India, Australia, Afrika Kusini, Korea Kusini na Brunei ambayo ni mwenyekiti wa sasa wa Jumuia ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN.


logoblog

Thanks for reading Mawaziri wa G7 kujadili haki za binaadamu

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment