May 9, 2021

Rais Tshisekedi awasili Sudan kwa mazungumzo ya bwawa la umeme la Ethiopia

  Muungwana Blog 2       May 9, 2021

 


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, jana aliwasili nchini Sudan kwa mazungumzo juu ya ujenzi wa bwawa la umeme lenye utata la Ethiopia katika mto Nile. 

Ziara ya siku moja ya Rais Tshisekedi inakuja wakati Sudan na Misri zikiishinikiza Ethiopia juu ya makubaliano ya lazima ya oparesheni za bwawa hilo kubwa la umeme la Ethiopia. 

Mwezi uliopita Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilikuwa mwenyeji wa mazungumzo baina ya nchi hizo tatu lakini mazungumzo hayo yalimalizika bila ya makubaliano. 

Wakati huo huo pia mjumbe maalumu wa Marekani katika pembe ya afrika Jeffrey Feltman alifanya mazungumzo jana na maafisa waandamizi wa Sudan.


logoblog

Thanks for reading Rais Tshisekedi awasili Sudan kwa mazungumzo ya bwawa la umeme la Ethiopia

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment