Ticker

6/recent/ticker-posts

Spika Ndugai amuonya Nape kuhusu michango yake bungeni

Spika wa Bunge,  Job Ndugai amemuonya mbunge wa Mtama (CCM),  Nape Nnauye kuchunga kauli zake anapochangia bingeni kuhusu wanawake.

Ametoa onyo hilo leo Jumatatu Mei 3,  2021 alipozungumzia  mchango wa mbunge huyo kuhusu wabunge 19 waliofukuzwa uanachama Chadema lakini bado ni wabunge.

Hivi karibuni Nape alikosoa wabunge hao kuendelea na nafasi zao licha ya kufukuzwa Chadema,  akitaka katiba ya nchi ifuate kumaliza hatima ya wabunge hao.

Leo Ndugai amemuombea msamaha Nape kwamba alikosea na watu wanatakiwa kumsamehe.

"Hivi karibuni mbunge wa Mtama mdogo wangu Nape Nnauye alitoa mchango wake hapa, Sina haja ya kuzuia uchangiaji wake lakini alikiuka kanuni kwa kuwataja wabunge kwa majina, hapo alikosea sana," amesema Spika Ndugai.

 

Post a Comment

0 Comments