Tetesi za soka Kimataifa

Leicester City na Everton ni miongoni mwa vilabu vinavyojiandaa na mchakato wa kumnasa mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney, 25. (Athletic)

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy atampa meneja ajaye wa klabu nafasi ya kumsainisha tena mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 31, kwa mkopo kutoka Real Madrid kwa msimu wa 2021-22.

Borrusia Dortmund itamuacha mchezaji wa kimataifa wa England Jadon Sancho kuondoka katika klabu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 87, baada ya hapo awali kutaka kiasi cha pauni milioni 100 kwa ajili ya kiungo huyo wa kati.

Mchezaji huyo, 21 amekuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia Liverpool na Manchester United.

Wakati huo huo Mtendaji Mkuu wa Dortmund Hans-Joachim Watzke amerejelea msimamo wa klabu kwamba mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United,Liverpool , Manchester City , Chelsea, Barcelona na Real Madrid- hatauzwa msimu wa joto. (Metro)


Newcastle United na klabu ya Italia, Atlanta zimeonesha nia hasa na mchezaji wa nafasi ya ulinzi ya Vitesse Arnhem Danilho Doekhi, 22, ambaye pia anahusishwa na taarifa za kutolewa macho na Norwich City, Fulham na mabingwa wa ligi ya primia ya Uskoti, Rangers. (De Telegraaf)


Wakala wa Robert Lewandowski Pini Zahavi anajiandaa kutia msukumo kwa Bayern Munich kumpa mkataba mpya mshambuliaji wa Poland au kumuuza katika klabu ambayo itaweza kummudu. (Bild-in German)

Watford wamefanya mawasiliano na Inter Milan na mlinzi wa England Ashley Young, 35, kuhusu kurejea kwenye klabu hiyo, ambako alianza kazi yake. (Watford Observer)


Familia ya Glazer inaweza kushawishiwa kuiuza Manchester United, lakini kiasi cha pauni bilioni 4 kinaweza kujaribu kuwashawishi. (Times, subscription required)

Klabu ya Ufaransa Nice imeendelea kuonesha nia ya kumsajili kiungo wa kati Jesse Lingard baada ya kumkosa alipojiunga kwa mkopo West Ham akitokea Manchester United mwezi Januari. (Sky Sports Italia)


Newcastle United ina nia ya kumuongezea mkataba mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Uswisi Fabian Schar,29, kabla ya michuano ya mabingwa Ulaya. (Northern Echo)

Tottenham imejaribu kufanya mawasiliano kwa ajili ya mchezaji wa Norwich na mlinzi wa England anayechezea kikosi cha umri wa chini ya miaka 21, Max Aarons, 21. (Football Insider


Boca Juniors wamemkosa mshambuliaji wa Manchester United na Uruguay Edinson Cavani, 34, na tayari wameweka nia ya kumpata mshambuliaji wa Club America wa miaka 26 Roger Martinez kama mbadala . (TyC Sports, via ESPN-in Spanish)


Lucas Vazquez anakaribia kuongeza mkataba wake na Real Madrid, lakini kuhamia AC Milan bado ni chaguo wakati wa majira ya joto ikiwa masharti hayatakubaliwa baada ya winga huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 29 kukataa.






 

Post a Comment

0 Comments