TGNP kwa kushirikiana na Wadau wamwagia sifa Rais Samia Suluhu Hassani kudumisha Demokrasia


Na Timothy Itembe Mara.

Mtandao wa wanawake katiba na uongozi na uchaguzi kwa kushirikiana na wadau wengine wanaoshugulika na maswala ya usawa wa njia na haki za wanawake wamechukua hatua ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani katika kuandika historia katika Tanzania na usawa hususani wa kijinsia.

 Akiongea kwa niaba ya wengine Lilian Liundi Mkurugenzi Mtendaji TGNP kwa niaba ya mtandao wa wanawake katiba uchaguzi na uongonzi alisema kuwa wamefuatilia hotuba ya Samia Bungeni aliyoitoa kwa mara ya kwanza tangu aapishwe machi,19,2021 nakutoa mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha miaka mitano ijayo hotuba hiii meonesha vipaumbele ambavyo vimegusa maeneo mbalimbali ya maendeleo katika nchi yetu,

Liundi aliongeza kusema katika hotuba hiyo ilijaa maudhui kwa masilahi ya Taifa yakiwemo yale ya kuneemesha maisha, haki, na usawa katika makundi mbalimbali ya kijamii,Kipekee tumefurahishwa na Mheshimiwa RaisSamia kwa kuonesha bayana tunu za kuongozaTaifa ambazo zimejumuisha masuala ya haki,demokrasia,na usawa.Nimatumaini yetu kuwa tunu hizi muhimu zikidumishwa,kulindwa nakutetewa,zitatoa mwanga mkubwa katika kuongoza utekelezaji wa vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya sita,ambavyo vimejumuisha kukuza uchumi nakupambana na umasikini nchini,kupambana narushwa naubadhirifu wa mali ya uma, ulipaji wa kodi usio na bughudha,

"Kukuza na kuongeza tija katika sekta ya kilimo na mifugo kukuza ajira na mapato kwa kukuza na kulinda sekta ya madini utalii,viwanda na kwingineko kuendeleza nakukuza miundombinu mbalimbali, kuboresha na kuleta mapinduzi zaidi ya teknolojia,TEHAMA na mawasiliano kuongezea uwekezaji katika sekta za nishati elimu,afya(na haswa afya ya uzazi)kukuza na kudumisha misingi ya demokrasia amani na uhuru, na zaidi kuhakikisha misingi ya haki na sheria zinatumika kulinda wananchi tunapenda kusisitiza kuwa katika uchambuzi wetu kuhusu Hotuba hii ya kwanza ya Mhe. RaisSamia, unaonesha kuwa maeneo yote yaliyopewa kipaumbele katika Serikali ya keya natoa fursa kubwa ya kukuza maendeleo ya takayowafikia na kuwanufaisha wanawake, wasichana na makundi mengi mengi ya wa nyonge nchini kama utekelezaji wa vipaumbele hivi utajengeka na kutekelezeka katika misingi ya haki na usawa, ukiwemo usawa wa jinsia"alisema Liund.

Hivyo tunamuomba Rais katika kukutana na vyama vya siasa kuwe na msisitizo wa kuhakikisha mkakati wa usawa wa njinsia na demokrasia ndani ya vyama inatekelezwa kama ajenda yao kimkakati.

Naye Monica Sedere kutoka TGNP alisema kutumia mifano michache tunaonyesha jinsi maeneo aliyo ya bainisha yanayo toa frusa za kukuza misingi na matokeo ya maendeleo yatakayo sababisha kukuwa kwa misingi  inayojumuisha usawa wa kijinsia.

Sedere alitumia nafasi hiyo  kusema wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ahadi ya kulinda misingi ya Demokrasia na Uhuru wa watu pamoja na wanasiasa na vyombo vya habari katika utekelezaji wa hili tunaona  frusa kubwa ya kujenga misingi na mikakati ambayo haitaacha nyuma ushiriki na sauti za wanawake kama wanajamii wa Taifa hili.

Sedere aliongeza katika kipaumbele cha kuboresha sekta ya madini utalii na nyinginezo ni chakupongezwa sana kwa bahati mbaya kwa mda mrefu sekta hizi zimekuwa zikitoa kipaumbele na kuwanufaisha zaidi wanaume kuliko wanawake.

 Pia Sedere aliongeza kuwa matumaini ya wadau na kuwa utekelezaji wa ahadi awamu ya sita utatilia mkazo kuhakikisha kuwa wanawake wananufaika na frusa zitokanazo na sekta hizo Ambapo juhudi za kuboresha kilimo ili kufangamanisha meendeleo ya kilimo na viwanda kwa lengo la kuwezesha mazao ya kilimo yatumike kama mali ghafi za viwandani jambo hili litasaidia wakulima wakiwemo wakulima wanawake vijijini kuweza kuuza mazao yao viwandani na kununua bidhaa za viwandani.

Kutoa kipaumbele katika uwekezaji na umiliki wa ardhi ni suala nyeti na tete ambalo linahitaji umakini mkubwa tunampongeza Rais kuainisha kipaumbele hiki na kuahidi kuwa ushiriki wa wanawake katika suala hili ni wa mhimu sana kwani ardhi imekuwa msingi mkuu wa ushiriki wa wanawake katika maendeleo tunatarajia kwamba wanawake ambao wamekuwa wakilisha Taifa hili kwa mda mrefu watapewa kipaumbele katika frusa zitokanazo na kilimo cha biashara tofauto tofauti na walivyokuwa wakiachwa nyuma aliongeza kusema.  

 Kuongeza usawa wa kijinsia kwa kuongoza wanawake wengi zaidi katika nafasi za Uongozi kwa kuzingatia vigezo na sifa stahiki juhudi hizi zitapunguza pengo la usawa wa kijinsia katika sera bajeti mipango na michakato yote ya maendeleo hii itasaidia katika kuongoza kasi ya maendeleo jumuishi na maendelevu nchini.

 Pia katika Kuongeza juhudi katika kupunguza vifo vya kina mama waja wazito na watoto.kuimarisha huduma za afya kwa kujenga miundombinu, kuongeza watumishi, vifaa-tiba, dawa na vitenganishi, pamoja na kuboresha Bima ya afya kwa wazee na kwa woteJuhudi hizi zita wasaidia wanawake ambao ndio wabeba mzigo mzito katika masuala ya afya katika familia na jamii kwa ujumla.

 Kuongeza uwajibikaji wa watendaji katika miradi ya maji, kuhakikisha upatikanaji wa maji sehemu zisizo na maji kwa kupitia mabwawa ya kuvuna maji ya mvua na kuimarisha kamati za maji za mitaa na vijiji il viweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisiJuhudi hizi zitawapunguzia wanawake mzigo wa kutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kutumia muda huo kwenye shughuli za uzalishaji alisema Sedere.

 Eneo la kuboresha mfumo wa elimu nchini kwa kufanya mapitio ya Sera ya Elimuna Ufundi ya mwaka 2014 na mitaaala ya elimu ili iendane na muktadha wa sasa. Tunatarajia mapitio haya ya takuwa jumuishi na yatatoa kipaumbele kwa watoto wakike na wenye ulemavu ili waweze kunufaika na haki yao ya msingi ya kupata elimu bora.

Sisi wana mtandao tunaahidi kuendelea kufanya kazi na Serikali ya Awamu ya Sita kwa njia mbalimbali ikiwemo kutoa ushirikiano kwa Mheshimiwa Rais wa JamhuriyaMuungano wa Tanzania na Serikali ya Awamu ya Sita katika kufuatilia nakutoa ushauri juu ya utekelezaji wa vipaumbele vilivyo ainishwa katika hotuba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

 

Post a Comment

0 Comments