Walimu watakiwa kutumia muda wa michezo kukuza vipawa vya wanafunzi


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Walimu nchini wametakiwa kuutumia ipasavyo muda ambao umetengwa kwaajili ya michezo katika kuibua vipawa vya wanafunzi ili kuwajengea uwezo wa kujiajiri pindi wanapohitimu masomo yao kwa ngazi tofauti.

Wito huo umetolewa na mgeni rasmi Padre wa jimbo la Njombe INNOCENT CHAULA katika hafla ya tamasha la kubaini vipawa vya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Collegine iliyopo kijiji cha Ilunda wilaya ya Njombe,ambapo amesema kuwa masomo ya darasani pekee hayatoshi kuwajengea uwezo wa kujiajiri wanafunzi.

Aidha Padre Chaula amesema kuwa endapo muda ambao umetengwa kwaajili ya michezo ukatumiwa ipasavyo hasa katika kuibua vipawa vya wanafunzi,kuwashirikisha katika shughuli za ulimaji wa bustani za shule itawasaidia zaidi wanafunzi hao kujitambua na kujua namna sahihi ya kuishi pindi wanapohitimu elimu yao.

“Mwanafunzi halelewi tu kwa kusoma vitabu,lazima ajifunze namna ya kusoma,kujitegemea lakini pia ni katika burudani na michezo ni vema mwanafunzi awe na zile stadi anazoweza kuishi nazo hata katika jamii”alisema Padre Chaula

Wakizungumzia kuhusiana na tamasha la kubaini vipawa vya wanafunzi wa shule hiyo ya collegine mwalimu wa shule hiyo FRANCE KIHOMBO na sister NOELA FEDRICK wamesema kuwa kupitia tamasha hilo wamebaini vipawa mbalimbali vya wanafunzi wao ikiwemo kuimba na kuigiza.

“Michezo inamjengea motto hali ya kujiamini,kujenga kipaji chake kitu ambacho hapo baadaye kinaweza kuja kumletea manufaa kutokana na vipaji vile walivyo navyo”alisema mwalimu Kihombo

Hata hivyo wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa kufanyika kwa tamasha hilo kunawapa elimu sahihi ya namna ya kuishi mara baada ya masomo yao na kujiepusha na vitendo vya kujihusisha na mahusiano ya kimapendi pindi wakiwa shule.

“Manufaa ni kukuza vipaji vyetu lakini pia kupunguza mawazo yale tunayoweza kuwa nayo kwasababu michezo inatujenga kimwili na kiakili”walisema wanafunzi

Tamasha hilo limehusisha michezo mbalimbali ikiwemo,kukimbia umbali wa kilomita tatu,kukimbiza kuku ,kuimba,kuigiza na kucheza mpira wa mikono na migu

Post a Comment

0 Comments