China yafikisha bilioni moja, idadi ya waliochanjwa dhidi ya corona


China imetangaza leo kwamba imefikisha jumla ya watu bilioni moja ambao wamepewa chanjo dhidi ya COVID-19 kufuatia kampeni yake kubwa kabisa ulimwenguni ya utoaji chanjo.


Maafisa wa afya nchini humo wanapania kuchanja asilimia 40 ya idadi jumla ya watu nchini humo ambayo ni sawa na watu bilioni 1.4 ifikapo mwisho wa mwezi huu.


Baadhi ya mikoa inatoa chanjo bila malipo kama njia ya kuwahimiza watu kujitokeza kuchanjwa.Katika mikoa mingine kama Anhui ya kati watu wanapewa mayai bila malipo na katika maeneo mengine ya mji wa Beijing watu wanapewa vocha za kununua bidhaa.


Hayo yanajiri mnamo wakati nchini Brazil, idadi ya vifo kufuatia janga hilo imepita watu nusu milioni.Ulimwenguni kote, idadi ya vifo kutokana na janga la COVID-19 imepita milioni 3.8.

Post a Comment

0 Comments