Jun 11, 2021

Fahamu miji 10 bora kuishi duniani 2021

  Muungwana Blog 2       Jun 11, 2021

Auckland, New Zealand, imetajwa kuwa ndio miji bora zaidi kwa mtu kuishi duniani katika wakati huu wa janga la virusi vya Corona.

Tathmini ya miji bora iliyofanywa na kitengo cha masuala ya uchumi -Economic Exploration Unit (EIU), iliangazia miji 140 ikizingatia masuala kama vile utulivu, elimu na upatikanaji wa huduma za afya.

Hatahivyo janga la virusi vya corona limekuwa kigezo kikuu katika tathmini ya miji ya mwaka huu na jinsi majukumu yanavyogawanywa.

Katika tathmini hiyo Ulaya imeonekana kushuka katika kiwango chake cha awali huku miji ya Australia na Japan pamoja na New Zealand ikipanda zaidi kwenye nafasi bora.

Mataifa haya yaliyoko katika maeneo ya theluji yalishughulikia haraka mlipuko wa virusi vya corona na yaliweza kupunguza idadi ya watu wanaoambukizwa na kulegeza masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.

Mataifa ya Muungano wa Ulaya, wakati huo huo, yalichelewa kuanza kutoa chanjo, na mataifa mengi ya Ulaya yaliweka masharti makali ambayo yameifanya miji hiyo kufanya vibaya katika utafiti wa mwaka huu wa miji bora zaidi ya kuishi duniani.

Auckland ilichukua nafasi ya kwanza ya orodha ya miji bora zaidi duniani, Osaka Japan ukawa wa pili na mji wa tatu ukawa wa Australia- Adelaide.

Miji ya Wellington wa New Zealand na Tokyo nchini Japan ilishika namba nne.

Nchini Uingereza hakuna mji hata mmoja ulioingia nafasi 10 za kwanza.

"Kupanda kwa mji wa Auckland kumetokana na kufanikiwa kwa mbinu yake ya kukabiliana na Covid-19, ambapo iliruhusu watu kuwa wazi zaidi kuhusu janga hilo na mji ulikuwa na mchango bora katika kuzuia maambukizi ," ilisema taarifa ya EIU.

"Miji ya Ulaya imefanya vibaya sana katika orodha ya mwaka huu ya miji bora ya kuishi," aliongeza.

Miji minane ambayo ilianguka kwenye orodha ya miji kumi bora ilikuwa ni ya miji ya Ulaya.

Kwa mfano, Mji wa Vienna Austria,umeshuka kutoka nafasi ya kwanza hadi nafasi ya 12.

Mji huo umekua ukiongoza kwenye orodha ya miji bora kwa miaka kadhaa, huku mji wa Melbourne ukiongoza.

Lakini mji wa Hamburg uliopo kaskazini mwa Ujerumani umeshuka sana kutoka nafasi ya 34 hadi ya 47

Orodha ya miji bora zaidi kuishi ni

Auckland, New Zealand

Osaka, Japan

Adelaide, Australia

Wellington, New Zealand

Tokyo, Japan

Perth, Australia

Zurich, Switzerland

Geneva, Switzerland

Melbourne, Australia

Brisbane, Australia

Orodha ya miji mibaya zaidi kuishi

Damascus, Syria

Lagos, Nigeria

Port Moresby, PNG

Dhaka, Bangladesh

Algiers, Algeria

Tripoli, Libya

Karachi, Pakistan

Harare, Zimbabwe

Douala, Cameroon

Caracas, Venezuela

 

logoblog

Thanks for reading Fahamu miji 10 bora kuishi duniani 2021

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment