Israel yakosoa kuchaguliwa kwa rais mpya mhafidhina wa Iran


Waziri Mkuu mpya wa Israel Naftali Bennett ameutaja ushindi wa kiongozi wa kihafidhina Ebrahim Raisi kuwa rais wa Iran, kama wito kwa pande zinazoshiriki mazungumzo ya kufufua mkataba wa nyuklia wa Iran kuzinduka.


Bennett ameliambia baraza lake la mawaziri leo kwamba kulingana naye kuchaguliwa kwa Raisi kunapaswa kuwa nafasi ya mwisho kwa nchi zenye nguvu kuzinduka na wafahamu ni mtu wa aina gani wanapofanya kazi naye.


Naye aziri wa mambo ya kigeni wa Israel Yair Lapid ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba rais mpya wa Iran ni mtu mwenye misimamo tete ambaye anahusishwa na vifo vya maelfu ya Wairan.Ameongeza kuwa Raisi anafahamika kama mchinjaji wa Tehran na kwamba kuchaguliwa kwake kunapaswa kuamsha juhudi mpya za dharura kukomesha mpango wa nyuklia wa Iran.


Raisi mwenye umri wa miaka 60 na ambaye ni mpambe wa kiongozi wa kidini Ayatollah Ali Khamenei na anayetuhumiwa na Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya kwa kukiuka haki za wanadamu, anatarajiwa kumrithi rais anayeondoka Hassan Rowhani.

Post a Comment

0 Comments