Jaji Mkuu Zambia afariki dunia


Siku chache baada ya kuondokewa na Mwasisi wa Taifa hilo, Hayati Dk. Kenneth Kaunda, Taifa la Zambia limempoteza tena Jaji Mkuu wake, Irene Chirwa Mambilima.

Taarifa iliyotolewa jana na Dk. Simon Miti ambaye Katibu wa Baraza la Mawaziri / Katibu Mkuu wa Rais imeeleza kuwa:

"Ni kwa masikitiko makubwa na huzuni kwamba Mheshimiwa Dk. Edgar Chagwa Lungu, Rais wa Jamhuri ya Zambia anangaza kwa taifa, kifo cha Jaji Irene Chirwa Mambilima, Jaji Mkuu wa Zambia kilichotokea Juni 20, 2021 saa 11:00 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya binafsi Mjini Cairo, Misri,"imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Jaji Mkuu alikuwa amesafiri kwenda Cairo Juni 10, 2021, kwa shughuli rasmi na aliugua akiwa kazini nchini humo.

Post a Comment

0 Comments