Lukuvi awapa rungu Makamishina wa Ardhi wa mikoa


Na Farida Saidy, Morogoro. 

Licha ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Samia Suruhu Hasan kulidhia kufuta mashamba 9 yenye ukubwa wa Hekari 13,900.5 Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro,Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi amewagiza Makamishina wa Ardhi Nchi nzima kufanya upekuzi wa mashamba makubwa yasio endelezwa.

Waziri Lukuvi alitoa maagizo hayo  Wilayani Mvomero mala baada ya kutangaza uamuzi wa Rais wa kufuta kwa mashamba hayo 9 na mashamba 86 yaliyopo Wilayani humo yanayotakiwa kufanyiwa upekuzi wa kina ili kujua uendelezaji wake na kama yanalipiwa kodi ili taarifa apelekewe Rais kuona kama yanahitajika kufutwa ama laa. 

Lukuvi alisema hayo wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero,Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji wa Wilaya hiyo,huku akisisitiza migogoro ya mipaka kati ya kijiji na kijiji kushughurikiwa na viongozi wa Wilaya na Mikoa.

“Natoa muda wa miezi miwili mwezi wa wasita na wasaba kwenye mashamba hayo 86 yaliyopo kwenye Wilaya hii yawe yamefanyiwa upekuzi na kuletewa taarifa juu ya mashamba haya.”alisema Waziri Lukuvi

Aidha Waziri Lukuvi akizungumzia namna ya mgawanyo wa Hekeri 13,900.5 Waziri huyo alisema mapendekezo ya Rais kuwa zaidi ya Hekari 9,700 zigawawiwe kwa Wananchi wa Wilaya ya Mvomero kwa ajili ya shughuri za kilimo na ufugaji na zigawiwe kwa makundi,huku Hekari 4,100 ziwe kwa ajili ya uwekezaji.

Akiwa katika kikao hicho ilijitokeza changamoto kati ya mwekezaji na wananchi wa Kata ya Doma kugombania kipande cha ardhi ambacho kinamilikiwa na mwekezaji aliyefahamika kwa jina la Alfa Haji lenye ukubwa wa Hekari 2,002.

Awali akitoa ombi la kusaidiwa kutatuliwa kwa mgogoro huo  baina ya mwekezaji na wananchi hao Diwani wa kata ya Doma Kristopher Maarifa alisema mgogoro huo umedumu zaidi ya miaka kumi na nyumba zaidi ya 60 zimejengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa Hekta 4 ambazo zipo barabarani.

Hata hivyo maamuzi ya Waziri baada ya kusikiliza pande zote mbili ameamulu mwekezaji kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mvomero ili kupata muafaka,huku akiagiaza eneo kupimwa na kupangwa.

Akizumza na mwekezaji kwa njia ya simu“nikueleze bwana Haji eneo hilo  litapangwa,tutapunguza hati yako na nyumba sitini hazita vunjwa”. “nimekusikia mkuuu hakuna linalo shindikana alisikika mwekezaji huyo”.

Pia katika kikao hicho mwananchi Abdu Ally(mlemavu)aliwasilisha malalamiko kwa Waziri ya kumegwa kwa eneo  yenye ukubwa wa Hekari saba kati ya 51anazozimiliki,ambapo maamuzi ya Waziri ni kurudishwa kwa eneo hilo kwa mlikiwake kama ilivyoamuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Albinus Mgonya hapo awali.

Awali kulikuwa na sintofahamu kati ya Afisa ardhi  Mkumbo Thomas na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero ya kwamba hekari hizo saba aachiwa mvamizi jamboo ambalo Ally aligoma kwa kuwa alikuwa na hatimiliki ya shamba hilo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mvomero Jonas Van Zeeland alimshukuru Rais na kwa kurejesha mashamba kwa wannchi yatakayowasaidia kutika kukuza uchumi wao na kupunguza migogoro ya ardhi wilayani huo.


 

Post a Comment

0 Comments