Maafisa biashara watakiwa kufikisha elimu ya usajili wa biashara kupitia mtandao kwa wananchi



Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wakalawa wa usajili wa Biashara na Leseni hapa Nchini Brela wametoa wito kwa maafisa biashara kufikisha elimu ya usajili wa biashara pamoja na upatikanaji wa leseni hizo kwa wananchi ili kuwapa fursa ya kutambua umuhimu wa leseni wanapohitaji kuingia katika biashara.

Brela wametoa wito huo kwa maafisa biashara wa wilaya na mikoa ya nyanda za juu kusini katika semina inayoendelea mkoani Njombe ili Kutoa Elimu Juu ya Kutambua Umuhimu wa Kusajili Biashara pamoja na upatikaji wa leseni kwa Wananchi.

Afisa Lesen mwandamizi kutoka Brela taifa Abas Cothema amesema Kutokana na adha Kubwa ambayo wananchi wamekuwa Wakikutana nazo wakati wa kusajili biashara zao pamoja na kupata leseni hapa Nchini brella imefikia hatua ya kutoa Elimu Kwa Maaifa Biashara wa mikoa ya Nyanda za Juu kusini lengo likiwa ni kutoa fursa kwa wananchi kupunguza mlolongo mrefu wa kupata huduma hiyo muhimu na kuisadia serikali kuingiza mapato pinda wananchi watakapo sajili biashara zao kwa wingi na kupewa Leseni.

"Maafisa wa biashara wao wako karibu sana na wafanyabiashara,leo tumetoa ellimu ni jinsi gani ya kuweza kuitambua na kuielewa sheria yetu ya leseni ya mwaka 1972 "alisema Abas Cothema

Kuhusu Wavumbuzi wa vitu mbalimvali nchini afisa Lesen Mwandamizi Brela Abas Cothema anasema tayari kuna mfumo mzuri ambao Brela imeweka ili kuwatambua na kuwapa haki zao pindi wanapo vumbua vitu mbalili.

"Na wiki iliyopita tuliweza kufanya mashindano ya uvumbuzi pale Dododoma na nia yetu ni kuweza kukusanya viapaji na kuendeleza haki za wavumbuzi wote ambao wanavumbua vitu mbali mbali hapa nchini"alisema tena Cothema

Baadhi ya Maafisa Biashara Kutoka Mikoa ya Njombe Iringa na Ruvuma akiwemo Martin Kabalo afisa Biashara wa mkoa wa Ruvuma na Zaituni Hamza afisa biashara wilaya ya Nyasa Wamekiri kupata elimu ambayo hapo awali ilikuwa Changamoto kwao na Kwamba  Tayari wanaenda kutimiza Wajibu wao wa kuwasogezea huduma hiyo muhimu Wananchi.

"Kabla ya mafunzo haya nilikuwa napitia chanagamoto kubwa sana hasa wakati wa kusajili majina ya biashara kwenye mfumo na kulzaimika kupiga simu ofisi za Brela Makao makuu ili watuelekeze baadhi ya hatu"alisema Martin Kabalo

Kuhusu changamoto ya Miundombinu ya Mawasiliano maafisa biashara wanakiri kuwepo kwa changamoto hiyo ,Lakini wanasema kwamba uwepo wa  usajili wa biashara na kupatiwa leseni mtandaoni imewapunguzia adha kubwa wananchi Ambao wamekuwa wakifuata huduma Hiyo Jijini Dar Es salaam.

"Chanagamoto ya kimfumo ni kweli ipo katika baadhi ya maeneo lakini kwa kiwango cha makao makuu ya halmashauri ipo mifumo ambayo tayari inafanya kazi vizuri"alisema Lusungu Mbede Afisa Biashara Mkoa wa Njombe

Post a Comment

0 Comments