https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mahakama ya rufaa DRC yadumisha hukumu dhidi ya Vital Kamerhe | Muungwana BLOG

Mahakama ya rufaa DRC yadumisha hukumu dhidi ya Vital Kamerhe


Mahakama ya rufaa mjini Kinshasa imedumisha hukumu ya mwezi Juni mwaka 2020 dhidi ya mkuu wa zamani wa wafanyikazi wa umma nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Vital Kamerhe, kwa wizi wa zaidi ya dola milioni 48 iliyokusudiwa kwa mpango wa kumuapisha Rais Felix Tshisekedi, wavuti ya Redio Okapi imeripoti.

Hata hivyo vifungo vya Kamerhe na watuhumiwa wenzake wawili vimepunguzwa. Kamerhe sasa atahudumia kifungo cha miaka 13 gerezani badala ya miaka 20.

Mfanyabiashara wa Lebanon Sammih Jamal amefungwa miaka sita, huku Jeannot Muhima, akihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja.

Post a Comment

0 Comments