Jun 10, 2021

Mwigizaji Kajala na mwanae waja na kipindi cha TV

  Muungwana Blog 2       Jun 10, 2021

 


Mwigizaji Kajala Masanja na Mwanae Paula wanatarajia kuja na kipindi cha Tv (Reality TV Show) yao itakayoitwa ‘Mom & Daughter, Like Twins’ na itakuwa ni mfululizo (series) wenye mkusanyiko wa matukio mbalimbali ya nyuma ya pazia katika shughuli zao za kila siku.


Kajala na Paula wame-share habari hizi njema kupitia kurasa zao za instagram kwa ku-post cover za ujio huo huku wakiacha ujumbe unaosema; 'Mom & Daughter "like twins" lifestyle reality show coming soon on your tv'.


Bado hawajaweka wazi ni kituo gani cha Tv ambacho kitarusha Reality show yao ya ‘Mom & Daughter, Like Twins’

logoblog

Thanks for reading Mwigizaji Kajala na mwanae waja na kipindi cha TV

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment