Jun 11, 2021

Naagiza mapato ya ndani asilimia 40 kupelekwa kwa Wananchi - RC Gabriel Robert

  Muungwana Blog 2       Jun 11, 2021


Na Timothy Itembe Mara.

Kabla ya aliyekuwa mkuu wa mkoa Mara,Gabriel Robert kuhamishiwa Mwanza kuotoka na mabadiliko madogo yaliyofanywa na Rais wa Jamuhuri ya muungano ya Tanzania Samia Suluhu Hssani aliitaka halamshauri ya Rorya kupeleka asilimia 40 ya mapato ya ndani kutekeleza miradi ya wananchi badala ya fedha hizo kutumika katika matumizi ya utawala na mambo mengine.

Robert alitoa kauli hiyo kwenye kikao cha baraza la madiwani chini ya mwenyekiti wake kilichoitishwa kwa lengo la kujadili Hoja za mkaguzi wa hesabu za serikali CAG kilichokalia ukumbi wa hoteli ya SOA.

Robert alisema amegundua kuwa katika hoja zinazopitiwa kujadiliwa na kupitishwa fedha ya makusanyo ya ndani ya asilimia 40 hazikupelekwa katika kutekeleza miradi ya wananchi badala yake zilitumika katika matumizi mengineyo.

Katika kikao hicho mkuu wa mkoa alihimiza madiwani pamoja na watendaji kuibua vyanzo vipya vya mapato ili kuwaletea fedh nyingi za kutekeleza miradi pamoja na hayo waimarishe vyanzo walivyo navyo vya makusanyo ya mapato ya ndani.

Naye mkurugenzi wa halmahauri ya Rorya,Charles Chacha alisema kuwa makusanyo ya mapato ya Rorya hayazidi milioni 800 kwa mwaka jambo ambalo linasababisha wakope fedha kutoka Amana ili hata kuendeshea vikao na kukabiliana na mabo kukwama.

Chacha aliongeza kusema maelekezo yaliyotolewa ikiwemo ushauri watauzingatia ili kuhakikisha wanajenga halmashauri hiyo.

Kwa upande wake mwenyekoiti wa halmashauri ya Rorya,Gerald Ng’ong’a , alisema kuna haja ya kutembelea vyanzo vya makusanyo walivyonavyo ikiwemo vikundi vya makundi maalumu ambavyo vinakopeshwa fedha ya makusanyo ya mapato ya ndani ili kujikwamua kimaisha.

"Kuna haja ya kutembelea vyanzo vyetu vya mapato ili kujiridhisha makusanyo tunayopata pamoja na hayo tutatembea kubaini vikundi vya wakina mama,Vijana na walemavu ambavyo vinapokea asilimia 10 ya mapato ya ndani ili kujiridhisha"alisema Ng'ong'a.

Syluana Didacus Ndemera wa kata ya Nyamtinga alisema kuwa halmashauri inatakiwa kuwashirikisha madiwani kujua vikundi ambavyo vinakokeshwa kwa kuwa vinatoka ndani ya kata wanazoziongoza.

Diwani huyo aliongeza kuwa madiwani wanavijua vikundi ambavyo vomi ndani ya kata kwa hali hiyo halmashauri ikileta mchanganuo na kuwashirikisha watafanikiwa katika swala zima la kukopa na kurejesha ili wengine wakope.

 

logoblog

Thanks for reading Naagiza mapato ya ndani asilimia 40 kupelekwa kwa Wananchi - RC Gabriel Robert

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment