Papa Francis atoa wito misaada iruhusiwe kupelekewa wakimbizi Myanmar


Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis amewahimiza viongozi wa kijeshi wa Myanmar kuruhusu misaada kupelekwa kwa watu ambao wanakabiliwa na njaa, baada ya kuyakimbia makaazi yao kutokana na machafuko ya tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa Februari mosi. Papa Francis aliwatolea wito viongozi hao pia kuheshimu maeneo na majumba ya kuabudu.


Amesema hayo mapema leo alipokuwa akiwabariki waumini katika viwanja vya kanisa la Mtakatifu Petero mjini Vatican. Wito wake unajiri wiki moja baada ya maaskofu wa kanisa Katoliki nchini Myanmar pia kutoa wito kama huo kwa wanajeshi. 


Papa Francis ambaye ametoa miito kadhaa kutaka wafungwa wa kisiasa wa Myanmar kuachiliwa huru alizungumzia kile alichokitaja kuwa masaibu ya kuvunja moyo yanayowakumba maelfu ya watu ambao walilazimika kuyakimbia makaazi yao na wanakufa kutokana na njaa nchini humo. 


Aliunga mkono maaskofu wa kikatoliki Myanmar, kutaka njia zifunguliwe kuruhusu misaada ya kiutu kuwafikia wakimbizi.

Post a Comment

0 Comments