Jun 11, 2021

Rawan Dakik ateuliwa kuwa Balozi wa hiari wa Mlima Kilimanjaro

  Muungwana Blog 2       Jun 11, 2021

Wizara ya Maliasili na Utalii imemteua Rawan Dakik kuwa balozi wa hiari wa Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kutambua jitihada zake za kutangaza Mlima Kilimanjaro, baada ya kupanda mlima huo kwa takriban mara tano na pia kuipeperusha bendera ya Tanzania katika kilele cha mlima mrefu zaidi duniani Everest uliopo bara la Asia.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Rawan Dakik yaliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro leo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akiteta jambo na wazazi wa Rawan kabla ya hafla fupi ya kumpokea iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Mhe. Mary Masanja pia amemtangaza Rawan Dakik kama Balozi wa hiari wa Mlima Kilimanjaro.


 

logoblog

Thanks for reading Rawan Dakik ateuliwa kuwa Balozi wa hiari wa Mlima Kilimanjaro

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment