Serikali mpya yaungwa mkono Algeria


Chama cha Ukombozi cha Kitaifa (FLN) ambacho kilishinda uchaguzi mkuu wa mapema uliofanyika tarehe 12 Juni nchini Algeria na kushinda viti 105, kilitangaza kuwa kiko tayari kuunga mkono serikali iliyoamuliwa na Rais Abdelmedjid Tebboune.

Katibu Mkuu wa FLN Abul Fadl Baji alitathmini matokeo ya uchaguzi katika mkutano na waandishi wa habari alioufanya kwenye makao makuu ya chama katika mji mkuu, Algiers.

Baji alijibu swali lililoulizwa juu ya aina ya serikali itakayoundwa kwa kusema,

"Mpango wetu uko karibu na ule wa Rais Tebboune, na kwa hivyo tunajiona katika serikali ya wengi ambayo Tebboune ataamua."

Baji pia alikumbusha kuwa mamlaka ya kuunda serikali iko mikononi mwa rais kama mlinzi wa katiba.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (ANIE) Mohammad Sharfi, ambaye alisimamia uchaguzi nchini Algeria, alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba FLN ilipata viti 105, vinavyolingana na asilimia 25.79 ya bunge lenye viti 407, na kuwa mshindi wa uchaguzi.

Akibainisha kuwa vyama vya kujitegemea vilishinda viti 78 sawa asilimia 19.16, chama cha Harakati ya Jamii ya Amani chenye mwelekeo wa Kiislamu kilishinda viti 64 sawa na asilimia 15.72, na chama cha Democratic National Unity (RND) kilishinda viti 57 sawa na asilimia 14, Sharfi pia alisema kuwa Mustakbel Front kilishinda viti 48 na Harakati ya Ujenzi wa Kitaifa kilishinda viti 40.

Sharfi alieleza kuwa  viti 15 vilivyobaki viligawanywa moja kwa moja kati ya vyama vingine vidogo,.

Post a Comment

0 Comments