Tetesi za soka kimataifa

 


Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo, 36, kwa mara nyingine tena hajakataa uwezekano wa yeye kutimka Juventus, kabla ya kumalizika kwa mkataba wake mwakani. Anahusishwa na klabu yake ya zamani ya Manchester United, huku Klabu hiyo ya Italia, ikitarajiwa kutengeneza pesa kupitia mkongwe huyo. (Express)

Winga wa England Jadon Sancho anatarajia kujiunga na Manchester United, licha ya Borussia Dortmund kukataa dau la awali la £67m kwa ajili ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 21. Klabu hiyo ya Bundasliga inang'ang'ania dau la £77m. (Manchester Evening News)

Chelsea wanapewa nafasi kubwa ya kumnasa kiungo wa England na Aston Villa, Jack Grealish msimu huu, wakitarajiwa kuzipiku klabu za jiji la Manchester, kwenye mbio za kupata saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25. (Fichajes via Mirror)

Uhamisho wa kiungo wa Switzerland Granit Xhaka kutoka Arsenal kwenda Roma inayonolewa na Jose Mourinho, hautarajiwi kukamilika mapema kwa sababu vilabu hivyo vimekutana na mkwamo katika mazungumzo ya uhamisho wa mchezaji huyo mwenye miaka 28. (Corriere dello Sport via Express)

Newcastle United imemuongeza mlinzi wa Liverpool Nat Phillips katika orodha ya wachezaji inaowafukuzia, lakini itawalazimu kupambana na Burnley kumnasa beki huyo wa kushoto raia wa Uingereza, ambaye hatarajii kupata nafasi watakapopona majeruhi Virgil Van Djik, Joe Gomez na Joel Matip. (Mail)

Mlinzi wa kushoto wa Arsenal na Scotland Kieran Tierney, 24, amehusishwa na uhamisho wa kuhamia Manchester City. Kocha wa zamani wa Celtic Neil Lennon, ndiye anayemuhusisha nyota huyo na uhamisho huo. (Times - subscription needed)

Mlinzi wa kati wa Real Madrid Raphael Varane anatarajia kutimka kwa wababe hao wa Hispania, huku vilabu vya Manchester United na Paris Saint Germain (PSG) vikionyesha nia ya kumtaka. Inaonekana nyota huyo mwenye miaka 28-angependelea kutua PSG ambao watalazimika kulipa kitita cha £51.5m kwa ajili ya mfaransa huyo. (El Confidencial, via Caught Offside)

Leicester City inatarajiwa kukamilisha usajili wa kiungo mfaransa Boubakary Soumare wiki hii. Vilabu vya Wolves na Everton navyo vinavutiwa na kinda huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye kwa sasa anachezea mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1) Lille. (Mail)

Mlinzi wa Burnley James Tarkowski anatarajiwa kutua West Ham msimu huu. Nyota huyo wa kimataifa wa England, mwenye umri wa miaka 28 amecheza michezo 36 msimu uliopita wakati Burnley ikinusurika tena kushuka daraja. (Football Insider)

Everton inamuwania nyota wa Sporting Lisbon Matheus Nunes, 22. Dau la kuanzia la £15m limetengwa kwa ajili ya kiungo huyo raia wa Brazil, dau linaloweza kufikia mpaka £17m ukijumlisha na masharti mengine. (Record, via Daily Star)

Post a Comment

0 Comments