Jun 11, 2021

Tetesi za soka kimataifa

  Muungwana Blog 3       Jun 11, 2021

 


Iwapo mazungumzo ya kumsajili winga wa England na Borrusia Dortmund Jadon Sancho ,21 yatagonga mwamba , Manchester United huenda ikamwinda Hudson Odoi , Dembele au kumsaini kiungo wa Portugal na Juventus Christiano Ronaldo.36. (Mail)

Chelsea inataka kumsaini beki wa kulia wa Inter milan na Morocco Achraf Hakimi . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akinyatiwa na klabu ya PSG.. (Times, subscription required).

Iwapo Chelsea itamsaini Hakimi basi wanaweza kusikiza ofa za kumuuza winga wa England Hudson Odoi 20 au Tino Livramento, huku Aston Villa ikiwa na hamu ya kumsajili beki huyo wa kulia. (Guardian)

Paris St-Germain inachunguza hali ya mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, ambaye kandarasi yake katika klabu hiyo ya Barcelona imesalia mwaka mmoja. (Marca)

Barcelona inafikiria kumsajili winga wa England na Manchester City Raheem Sterling ambaye anaonekana kama chaguo la kuchukua nafasi yake Dembele iwapo hataongeza kandarasi yake.

Meneja wa zamani wa Liverpool na Newcastle Rafael Benitez anawania umeneja wa Everton baada ya kazi hiyo kuachwa wazi. (Mail)

Mmiliki wa klabu ya Inter Miami Jorge Mas amethibitisha kwamba yeye na mmiliki mwenza wa klabu hiyo David Beckham wamekuwa na mazungumzo na mshambuliaji Muargentina Lionel Messi, 33, kuhusu kujiunga na timu hiyo kama sehemu ya mazungumzo ya mkataba na Barcelona wa miaka 10 wa mchezaji huyo nyota. (Miami Herald)

Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, ameweka sharti aliposaini mkataba mpya na PSG kwamba hawatamuuza mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, msimu huu. (AS - in Spanish)

Tottenham wanafanya mazungumzo na winga wa Borussia Monchengladbach Mfaransa Marcus Thuram - mwana wa kiume wa mshindi wa Kombe la Dunia Lillian - kabla ya uwezekano wa uhamisho msimu wa majira ya joto. (RMC Sport - in French)

logoblog

Thanks for reading Tetesi za soka kimataifa

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment