Watumishi hewa waliokwapua fedha za Halmashauri ya mji wa Tarime kusakwa


Na Timothy Itembe Mara.

Mkuu wa mkoa Mara,Gabriel Robert ameagiza kamati ya ulinzi na usalama kupitia mkuu wa wilaya Tarime kuwasaka na kukamatwa watumishi hewa taklibani watano ndani ya halmashauri ya mji wa Tarime ambao wanadaiwa kuchukua fedha kwanjia ya utapeli na kuzirudisha.

Robert alisema mbele ya kikao cha ukaguzi wa hesebu za serikali CAG kilichokalia ukumbi wa Tarime sekondari kwa ajili ya kujadili na kupitisha Hoja za mkaguzi wa hesebu za serikali CAG. katika halmashauri ya mji wa Tarime mkoani hapa.

"Niombe kamati ya ulinzi na usalama kupitia mkuu wake ,Mtemi Msafiri kuwasaka na kuwakamata watumishi hewa ambao wanadaiwa kuipelekea hasara halmashauri ya mji wa Tarime kwa kuchukua fedha kwanjia ya udanganyifu ambazo ni kodi ya maendeleo kwa wananchi na kutokomea nazo kusiko julikana"alisema Robert.

Mkuu huyo aliwataka watumishi kushirikiana na madiwani kusimamia fedha za serikali kwa kuzingatia ilani ya uchaguzi ya  Chama cha mapinduzi ya mwaka 2020/2025.

Akisoma hoja hizo mweka hazina wa halmashauri hiyo,Zubeda Nkala alisema kuwa watumishi hao wanadaiwa kuchukua fedha hiyo kati ya mwaka 2015 na 2016 na kuwa zaidi ya shilingi  milioni miambili arobaini na tano alfu na miatisa. zimepotea mifukoni mwao na watumishi hao hawajulikani walipo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya Tarime Mtemi Msafiri alimpongeza mkuu wa mkoa huyo na kuahidi kutekeleza maagizo kama yalivyotolewa kwa utekelezaji zaidi.

Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Tarime,Elias Ntiruhumgwa alisema yote yaliyoelekezwa watayafanyia kazi vizuri na kwa uharaka zaidi ili kutatua na kupunguza hoja za ukaguzi kwa kuzitafutia mikakati ya kuzipunguza kama sio kuzimaliza kabisa.

Post a Comment

0 Comments