Waziri Ummy Mwalimu amsimamisha kazi Mhandisi wa ujenzi mradi wa stendi ya mabasi Mwenge

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Mhe.Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi mhandisi Isack Mpaki anaesimamia miradi mitatu ya manispaa ya kinondoni ikiwemo Ujenzi wa Stendi ya Mabasi mwenge, Ujenzi wa Uwanja wa Mpira Mwenge na Ujenzi wa Jengo la Utawala la Manispaa ya Kinondoni baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa mradi huo.


Waziri Ummy amechukua hatua hiyo leo Juni 20, 2021 mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi wa Stendi ya Mabasi Mwenge Jijini Dar es Salaam ambapo ujenzi huo unajengwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa mfumo wa Local Fundi ( Force Account) ulianza Aprili mwaka mwaka jana ambapo pamoja na mambo mengine utaiwezesha Manispaa kukusanya mapato.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo Waziri Ummy amesema kuwa ili aweze kujiridhisha ni lazima kuundwe timu ambayo itaweza kuchungunza ujenzi wa mradi huo ili aweze kutoa tmko rasmina ujenzi ukaendelea.

Aidha Waziri Ummy amesema amepata malalamiko na jumbe nyingi kutoka kwa wakazi wa manispaa ya Kinondoni hususani wananchi ambao walikuwa wanatumia eneo hilo  wakilalamika kusuasua kwa ujenzi wa stendi ya mwenge ya mabasi ambao ulikuwa umalizike Mei 2 mwaka huu.

“Kuna figisufigisu kwenye huu mradi haiwezekani tukawa tunatupiana mipira kwahiyo  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Prof.Shemdoe nataka Jumanne aniletee timu huru ya kuja kuchunguza mikataba yote”. Amesema Waziri Ummy.

 

Post a Comment

0 Comments