Jul 21, 2021

Israel yatakiwa kutouza teknolojia ya udukuzi

  Muungwana Blog       Jul 21, 2021


Shirika la waandishi habari wasio na mipaka, RSF limeitaka Israel kuacha kuuza teknolojia ya udukuzi, wakati ambapo kuna madai ilitumika kuwalenga wakuu kadhaa wa nchi na mamia ya waandishi habari.


 Mkuu wa shirika hilo, Christophe Deloire amesema wanamtaka Waziri Mkuu wa Israel, Naftali Bennett kusitisha mauzo ya teknolojia ya ujasusi hadi mfumo wa udhibiti utakapowekwa. 


Wito huo umetolewa baada ya namba za simu zipatazo 50,000 kuvuja, ambazo zinaaminika zilikuwa kwenye orodha ya kudukuliwa na kampuni ya Israel ya teknolojia ya ujasusi ya NSO. Orodha hiyo inajumuisha wakuu 14 wa nchi akiwemo Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron. NSO imesema ina mikataba na nchi 45 na kwamba wizara ya ulinzi ya Israel lazima iidhinishe mikataba hiyo. 


Magazeti ya The Gurdian, Le Monde na The washington Post yaligundua takriban waandishi habari 200 walikuwa kwenye orodha hiyo.

logoblog

Thanks for reading Israel yatakiwa kutouza teknolojia ya udukuzi

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment