Jul 21, 2021

Maambukizi ya COVID-19 yaongezeka Ujerumani

  Muungwana Blog       Jul 21, 2021


Idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya corona kwa wakaazi 100,000 ndani ya siku saba yameongezeka kwa kasi kwa zaidi ya wiki mbili. 


Kwa mujibu wa taasisi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza Ujerumani, Robert Koch kiwango kilikuwa ni 11.4 ikilinganishwa na siku iliyotangulia iliyokuwa 10.9 na kiwango cha chini kabisa kilikuwa 4.9 tarehe 6 ya mwezi huu wa Julai. 


Kulingana na takwimu mpya, vifo 19 vimerekodiwa Ujerumani ndani ya saa 24. Wakati huo huo, kampuni za kutengeneza chanjo ya COVID-19 ya BioNTech na Pfizer zimesema kuwa zimempata mshirika wa Afrika Kusini kwa ajili ya kutengemeza chanjo hiyo itakayokuwa mpango wa kwanza barani Afrika.


Kampuni hizo zimesema leo kuwa chini ya makubaliano, kampuni ya Biovac yenye makao yake mjini Cape Town itakamilisha hatua za mwisho za mchakato wa utengenezaji wa chanjo ya BioNTech-Pfizer.

logoblog

Thanks for reading Maambukizi ya COVID-19 yaongezeka Ujerumani

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment