Mahujaji waelekea Mlima Arafat Makka


Mahujaji wa Kiislam nchini Saudi Arabia leo wamekusanyika katika eneo la Minna katika mlima Arafat ikiwa ni siku ya pili na muhimu ya ibada ya Hijja inayofanywa kwenye mji mtakatifu wa Makka. 

Ni waislamu 60,000 tu, ambao ni raia au wakaazi wa Saudi Arabia, waliochaguliwa kushiriki, na raia wa kigeni wamezuiliwa kwenda Hijja kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na janga la virusi vya corona.

 Baada ya sala ya adhuhuri, waumini hao wa Kiislam watapanda kwenye mlima Arafat wa mita 70 na hapo wataswali, watasoma Quran, na kutubia makosa yao kwa Mola wao hadi jioni. 

Baada ya jua kuzama wataelekea Muzdalifah, eneo lililoko kati ya Arafat na Minna, na huko watalala na baadae kuamka kwa ajili ya kumpiga mawe shetani kwenye nguzo tatu zilizomithilishwa na shetani, ambao ni utaratibu wa mwisho wa ibada ya hijja.

Post a Comment

0 Comments