Jul 19, 2021

Makambo aagwa rasmi Horoy

  Muungwana Blog 3       Jul 19, 2021

 


KLABU ya Horoya  iketangaza rasmi kusitisha mkataba na mchezaji wao Heritier Makambo.

Kupitia katika ukurasa rasmi wa Horoya ya Guinea wameandika kwamba wanashukuru kwa huduma ya mchezaji huyo ambaye amedumu hapo kwa muda wa misimu miwili.

Nyota huyo aliibuka hapo akitokea Klabu ya Yanga ambapo alikuwa ni mfungaji namba moja Yanga alipotupia mabao 17 na kuwa namba tatu kwa washambuliaji wenye mabao mengi.

Huenda dili lake la kurudi Yanga likajibu kwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi hao ambao wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya pili.

Hivyo kuangwa kwake rasmi na mabosi wake hao kunafanya dili lake kuwa jepesi kuweza kutua Yanga.

logoblog

Thanks for reading Makambo aagwa rasmi Horoy

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment