Jul 21, 2021

Msaidizi wa Trump ashtakiwa kwa kuwa wakala wa UAE

  Muungwana Blog       Jul 21, 2021

 


Mwenyekiti wa kamati iliyosimamia kuapishwa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump mwaka 2017, amekamatwa kwa madai ya kujaribu kushawishi sera za kigeni za Trump kuupendelea Umoja wa Falme za Kiarabu. 


Thomas Joseph Barrack wa Santa Monica, California, mwenye umri wa miaka 74 alikuwa miongoni mwa wanaume watatu walioshtakiwa katika mahakama ya New York kwa kujaribu kushawishi sera za kigeni wakati Trump anagombea urais mwaka 2016 na baadae akiwa rais. Barrack anashtakiwa kwa kula njama, kuzuia haki na kutoa taarifa za uongo kwa maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI Juni 20, mwaka 2019. 


Mahakama ya Shirikisho ya Brooklyn pia imemshtaki Matthew Grimes wa Aspen, Colorado na Rashid Sultan RAshid Al malik Alshahhi wa Umoja wa Falme za Kiarabu.

logoblog

Thanks for reading Msaidizi wa Trump ashtakiwa kwa kuwa wakala wa UAE

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment