Tetesi za soka kimataifa


Aston Villa wanatarajiwa kuanza tena mazungumzo na kiungo wa England Jack Grealish, 25, wiki ijayo na wako tayari kumpa mkataba mpya wa kuzuia hamu kutoka kwa Manchester City. (Express na Star)

Mabingwa wa Ligi ya Premia City, hata hivyo, wameanza mazungumzo na Villa kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo - na uamuzi kuhusu ikiwa makubaliano ya Grealish yanaweza kuafikiwa utafanywa ndani ya siku chache. (Guardian)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anatarajia kufanikisha usajili wa Grealish kwa wakati kabla ya mechi za Community shield tarehe 7 Agosti (Star)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 28, ameweka wazi kuwa ana nia ya kusalia na mabingwa wa Italia Inter Milan baada ya kukataa ofa ya kurudi Chelsea. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Wakala wa Paul Pogba Mino Raiola amemkabidhi kiungo huyo wa kati wa Manchester United na Ufaransa, 28, kwa Liverpool. (Le 10 Sport - in French)

West Ham wanaandaa dau la pauni milioni 20 kwa Kurt Zouma, 26, wa Chelsea, ambaye anasemekana anapendelea kuhamia London badala ya kutumiwa katika makubaliano na Sevilla kwa beki mwenzake Mfaransa Jules Kounde, 22(Mail)

Mlinda mlango wa Manchester City mwenye umri wa miaka 27 Ederson anatarajiwa kuongezewa mkataba wa miaka mitatu(Athletic - subscription required)

Kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger amehusishwa na nafasi iliyo wazi ya kocha wa Uswizi. Mfaransa huyo hajafanya kazi katika usimamizi tangu kuiongoza Arsenal kwa miaka 22 hadi 2018. (Blick, via Mail)

Mlinzi wa Marekani Sergino Dest, 20, ameamua kubaki Barcelona na amekataa uhamisho wa kwenda vilabu vya Arsenal, Bayern Munich na Borussia Dortmund. (ESPN)

Afisa mkuu Mtendaji wa Sassuolo Giovanni Carnevali amesema watakubali tu kumuuza kiungo wa kati wa Italia mwenye umri wa miaka 23 Manuel Locatelli, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda Arsenal na Juventus, ikiwa ofa mwafaka itatolewa mapema kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho. (Gazzetta dello Sport, via Mirror)

Mlinzi wa Atletico Madrid na England Kieran Trippier, 30, anatarajia uhamisho wake kwenda Manchester United utachukua hadi mwisho wa dirisha la uhamisho kufaulu . (Manchester Evening News)

Arsenal wako tayari kusikiliza ofa kwa winga wa Brazil mwenye umri wa miaka 32 Willian wanapojaribu kupunguza kiasi cha fedha wanzzotoa kama mishahara kwa wachezaji wao (Star)

Real Madrid itakuwa tayari kumruhusu kiungo wa Norway Martin Odegaard aondoke kwa karibu pauni milioni 43, na Arsenal inamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 baada ya kipindi chake cha mkopo Kaskazini mwa London msimu uliopita. (ESPN)

AC Milan wamemfanya winga wa Chelsea mwenye umri wa miaka 28 raia wa Morocco Hakim Ziyech kuwa lengo lao kubwa wakati wanapolenga kuimarisha safu yao ya ushambuliaji (Calciomercato - in Italian)

Aston Villa wanajiandaa kuanza mazungumzo na kipa Emiliano Martinez kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu baada ya juhudi zake katika kuisaidia Argentina kushinda Copa America kuzua hamu mpya kwa mchezaji huyo wa miaka 28. (90min)

Torino wamewasilisha ofa "kubwa sana" ya kuongeza mkataba kwa mshambuliaji wa Italia Andrea Belotti, 27, wakati wanajaribu kuzuia Roma na Arsenal kumchukua mchezaji huyo (Tuttomercatoweb, via Goal)

Mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema, 33, anatarajiwa kusaini mkataba mpya na Real Madrid, hatua itakayomfanya kusalia mji mkuu wa Uhispania hadi msimu wa joto wa 2023. (Marca - in Spanish)

Watford watamchukua kiungo wa miaka 24 wa St Mirren wa Jamhuri ya Ireland James McGrath ikiwa watashindwa katika juhudi zao za kumsaini Lewis Ferguson wa miaka 21 kutoka Aberdeen. (Sun)

Newcastle United imeipiku Aston Villa katika jitihada za kumsajili beki wa zamani wa England wa chini ya umri wa miaka 21 Axel Tuanzebe, 23, kwa mkopo kutoka Manchester United msimu huu wa joto.

 

Post a Comment

0 Comments