Tetesi za Soka kimataifa


 Chelsea imezengumza na ajenti wa mshambuliaji wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland Robert Lewandowski, 32, kuhusu uwezekano wa kumleta Stamford Bridge. (Bild, via Sun)

Arsenal inajiandaa kuwasilisha dau la pauni milioni 30 kumnunua kipa wa Sheffield United Muingereza Aaron Ramsdale, 23. (TalkSport)

Gunners hata hivyo wametakiwa kuongeza ofa ya Ramsdale kwa zaidi ya pauni milioni 32 baada ya ofa zao mbili za awali kukataliwa. (Times)

Chelsea wako tayari kumuachilia mshambuliaji Tammy Abraham kujiunga na mahasimu wao wa Ligi ya Premia Arsenal kwa mkopo. Tottenham na West Ham pia wanamnyatia kungo huyo matata aliye na umri wa miaka 23. (Sun)

Mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 25, ameanzisha mazungumzo ya kuondoka Chelsea msimu huu wa joto. Kuna uwezekano akarejea katika ligi yake nyumbani Bundesliga. (90min)

Liverpool huenda wakamuuza mchezaji wa safu ya kati na nyuma Nat Phillips, 24, winga wa Wales Harry Wilson, 24, Mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, 26, beki wa Wales Neco Williams, 20, na kiungo wa kati wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 29, katika mpango wa kukusanya kati ya paundi milioni 60-70. (Liverpool Echo)

Paris St-Germain wanamtaka kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28, lakini klabu hiyo ya Ufaransa itahitajika kuwauza baadhi ya wachezaji wake kwanza. (Sky Sports)

Manchester United wako mbele ya Arsenal mchakato wa kumsajili kiungo wa kati wa Portugal Ruben Neves, 24, kwa kima cha paundi milioni 35 kutoka Wolves msimu huu wa joto. (TalkSport)

United wamempatia kiungo wa kati wa Ujerumani Leon Goretzka ofa ya paundi elfu 200-kwa-wiki kumasaini wakati mkataba wa nyota huyo wa miaka 26-utakapokamilika Bayern Munich msimu ujao(Daily Mail)

Manchester United wamempatia kiungo wa kati wa Ujerumani Leon Goretzka ofa ya £200k-kwa-wiki kumasaini

Lakini Real Madrid pia wamewasiliana Gortezka kuhusu uwezekano wa kumnunua. (Bild, via Marca)

Aston Villa wamepiga hatua katika mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Norwich City aliye na miaka 23 Todd Cantwell. (Football Insider)

Wachezaji wa soka waliohamia kutoka klabu moja hadi nyengine Ulaya

Villa pia wako tayari kumnunua winga wa Bayer Leverkusen Mjamaica Leon Bailey,23, ambaye thamani yake inakadiriwa kiwa kati ya £25m-£30m. (Daily Mail)

Crystal Palace wanajadiliana na Schalke kuhusu mkataba wa mlinzi wa Uturuki Ozan Kabak, 21. Huenda akagharimu kati ya pauni milioni 10-12. (Guardian)

Everton imeungana na orodha ya klabu zinazofuatilia hali ya mshambuliaji Jesse Lingard ,28, Manchester United. (Sun)

Meneja wa West Ham David Moyes atamgeukia kiungo wa kati wa Chelsea Muingereza Ross Barkley, 27, ikiwa klabu hiyo itashindwa kumsajili Lingard. (90min)

Mwamuzi wa kwanza wa kike kuvaa hijab katika historia ya Olimpiki

Newcastle ina matumaini ya kuafikiana na Southampton kuhusu mkataba wa pauni milioni nne wa kiungo wa kati wa Gabon Mario Lemina, 27,wiki hii. (Daily Mail)

Kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 24, amedhamiria kubaki Manchester United msimu huu wa joto licha ya kutakiwa na klabu za Italia, Uhispania na Ujerumani. (Manchester Evening News)

Leeds United wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Muingereza Lewis Bate,18. The Blues wanatarajiwa kujumuisha kifungu cha sheria kitakachoongoza kuuzwa kwake lakini sio cha kumnunua tena akiondoka. (Leeds Live)

Juventus wanakaribia kufikia makubaliano na klabu ya Sassuolo nchini Italia kumhusu mchezaji Manuel Locatelli, 23. (Corriere dello Sport - in Italian)

Barcelona inakabiliwa na hali ngumu ya kifedha na huenda ikalazimika kupunguza mishahara ya thamani ya euro milioni 441 ili kufikia viwango vya mishahara vilivyowekwa na La Liga(Star)

Post a Comment

0 Comments