Ubelgiji yakaa kimya kwa heshima ya wahanga wa mafuriko

 


Ubelgiji imekaa kimya kwa dakika moja leo Jumanne kama ishara ya kuwakumbuka wahanga wa mafuriko yaliosababisha vifo vya watu wapatao 200 magharibi mwa Ulaya.


Watu wasiopungua 31 wamefariki nchini Ubelgiji pekee, huku mamia ya wengine hawajulikani waliko wakati nchini Ujerumani, watu 165 wamefariki huku shughuli ya uokoaji ikiendelea.


Mvua kubwa zilizoandamwa na mafuriko zilifanya ubaribifu mkubwa katikati mwa miji na vijjii hasa nchini Ubelgiji na Ujerumani ambapo Kansela Angela Merkel amefanya ziara kuwatembelea wahasiriwa wa mafuriko hayo katika mji wa Bad Munstereifel.Idadi ya watu waliopotea nchini Ubelgiji imepungua katika muda wa siku mbili zilizopita baada ya huduma za mawasiliano kurudi tena na watu zaidi wanafuatiliwa.


Mfalme wa Ubelgiji Phillipe na Malkia Mathilde wametembelea kituo cha wazima moto cha Verviers, mojawapo ya miji iliyoathirika zaidi na mafuriko.

Post a Comment

0 Comments