Jul 21, 2021

UN: zaidi ya wahamiaji 500 wakamatwa ndani ya saa 24

  Muungwana Blog       Jul 21, 2021


Shirika la Umoja wa Mataifa la Wahamiaji, IOM, limesema leo kuwa wahamiaji wapatao 20 wamezama na wengine zaidi ya 500 wamekamatwa ndani ya muda wa saa 24 katika Bahari ya Mideterania. Shirika hilo limesema wahamiaji hao wamerejeshwa Libya. 


Msemaji wa IOM, Safa Msehli ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba wahamiaji walikamatwa na wote wanashikiliwa. Hakufafanua zaidi kuhusu watu 20 waliozama. 


Zaidi ya wahamiaji 14,700 wamekamatwa na walinzi wa pwani wa Libya wanaoungwa mkono na Umoja wa Ulaya katika nusu ya kwanza ya mwaka huu. 


Umoja wa Mataifa umesema idadi hiyo ni zaidi ya waliokamatwa mwaka wote wa 2020. Umoja wa Mataifa na mashirika ya kutetea haki za binaadamu yamerudia kutoa onyo kwamba wahamiaji wa Libya wako katika hatari ya kuteswa, kunyanyaswa kingono na usafirishaji haramu wa binadamu.

logoblog

Thanks for reading UN: zaidi ya wahamiaji 500 wakamatwa ndani ya saa 24

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment