Urusi kutotumia nishati yake kama silaha ya kisiasa

 


Urusi imesema haitotumia nishati yake kama silaha ya kisiasa. Matamshi hayo yametolewa leo na Ikulu ya Urusi wakati ikitoa maoni kuhusu mradi wenye utata wa bomba la gesi unaogharamiwa na Urusi na Ujerumani unaojulikana kama Nord Stream 2. 


Marekani na Ujerumani zimeahidi kuchukua hatua dhidi ya Urusi, iwapo italitumia bomba hilo la gesi kuiumiza Ukraine au mataifa mengine ya Ulaya Mashariki. Taarifa hizi ni kulingana na vyanzo viwili vilivyo karibu na makubaliano ya pande mbili yanayotarajiwa kufikiwa leo. Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema Ukraine itabakia kuwa njia ya kupitisha gesi asilia. 


Merkel amesema kinyume na hili itasababisha mvutano mkubwa. Kansela huyo wa Ujerumani amesisitiza kuwa watachukua hatua iwapo Urusi haitoheshimu haki ya Ukraine kuwa nchi inayopita gesi hiyo.

Post a Comment

0 Comments