https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mawaziri wa EU kuujadili mzozo wa AUKUS | Muungwana BLOG

Mawaziri wa EU kuujadili mzozo wa AUKUS

 


Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kujadiliana kuhusu ushirika mpya wa kijeshi kati ya Marekani, Uingereza na Australia uliopewa jina AUKUS ambao umeufuta mkataba kati ya Australia wa kununua nyambizi za Ufaransa. 

Msemaji wa masuala ya kigeni ya Umoja wa Ulaya, Peter Stano amesema mkutano huo utafanyika pembezoni mwa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New Yoek, Marekani. 

Stano amesema hiyo ni fusra ya kwanza kwa mawaziri wa Umoja wa Ulaya kujadili athari ya mkataba huo, sio tu kwa suala kati ya Ufaransa na Australia, lakini pia matokeo ya mkataba wote wa AUKUS.


Post a Comment

0 Comments