Rusesabagina ahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela

 


Baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki katika vitendo vya ugaidi, aliyekuwa shujaa wa filaumu ya Hotel Rwanda Paul Rusesabagina hatimaye amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela.

Mahakama moja nchini Rwanda ilimpata na hatia kuhusiana na mashtaka yanayohusiana na ugaidi.

Alisusia uamuzi wa kesi hiyo na hakutoka jela ili kuhudhuria mahakama.

Rusesabagina alituhumiwa kwa kuwa mwanzilishi na mfadhili wa kundi moja la waasi ambalo lilitekeleza mashambulio nchini Rwanda 2018 na kuwaua watu tisa.

Mkosoaji huyo wa Rais Paul Kagame alikiri kutuma fedha kwa kundi hilo lakini akakana kuhusika katika mashambulizi.

Rusesabagina ametaka kesi hiyo kuwa aibu.

Mwanawe wa kike Anaise Kanimba aliambia BBC kwamba familia yake haijaamua iwapo itakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Post a Comment

0 Comments