https://monetag.com/?ref_id=TTIb Dunia yalaani mapinduzi ya kijeshi Sudan | Muungwana BLOG

Dunia yalaani mapinduzi ya kijeshi Sudan

 


Viongozi wengi wa dunia wamelaani mapinduzi ya kijeshi nchini Sudan, yaliyoiondoa madarakani serikali ya mpito na kumtia kizuizini waziri mkuu Abdalla Hamdok na viongozi wengine wa kiraia. 

Rais wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Mousa Fakki Mahamat amesema umoja huo umesikitishwa na hali inayoendelea nchini humo, na umehimiza mazungumzo ya haraka kati ya wanajeshi na raia. 

Mjumbe wa Marekani kuhusu Upembe wa Afrika Jeffrey Feltman amesema hatua hiyo ya jeshi inakwenda kinyume na matarajio ya kidemokrasia ya raia wa Sudan. 

Ujerumani kupitia waziri wake wa mambo ya nje Heiko Maas imesema jaribio la mapinduzi nchini Sudan ni hatua inayoleta wasiwasi, na kuwataka wote wenye dhamana ya usalama nchini humo kuhakikisha kuwa mchakato wa kuelekea demokrasia hautatizwi. 

Umoja wa mataifa ya kiarabu nao umetaka pande zote nchini Sudan kuendelea kuheshimu makubaliano ya kugawana madaraka ya Agosti mwaka 2019.


Post a Comment

0 Comments