https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mashambulio mapya ya ndege yapiga yapiga maeneo mapya Tigray | Muungwana BLOG

Mashambulio mapya ya ndege yapiga yapiga maeneo mapya Tigray

Serikali ya Ethiopia inasema kuwa jeshi limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya waasi kaskazinina magharibi mwa jimbo la Tigray -na kupanua wigo wa makombora yake ya anga.

Mashambulio ya awali ya snga kwa kipindi cha wiki iliyopita yalikuwa yanalenga katika mji mkuu wa jimbo Bekelle, lakini haya yamepiga katikaAdwa na Mai Tsebri.

Serikali ilisema kwamba yalikuwa yamelenga maeneo ya Tigray People's Liberation Front (TPLF) lakini raia kadhaa wameripotiwa kuuawa.

Msemaji wa TPLF alisema kuwa hakuna eneo la jeshi lililopijgwa na akasema makombora ya masafa yalipiga majengo ambayo tayari yalikuwa yameharibiwa na vikosi vya Ethiopia na Eritrea.

Huku mawasiliano yote ya simu yakiwa yamekatwa katika Tigrayitakuwa vigumu kuthibitisha athari za mashambulio ya anga-hususan kwamba maeneo hayo ni magumu kufikiwa.

Pia nyako mbali kutoka eneo ambako mapambano makali yamekuwa yakifanyika-karibu na jimbo la Amhara.

Baada ya karibu mwaka mmoja wa mzozo kati ya TPLF na vikosi vinavyoiunga mkono serikali , Umoja wa Mataifa unasema watu milioni saba wanahitaji msaada wa dharura na wengine zaidi ya milioni mbili wamesambaratishwa kutokana na mzozo huo.

 

Post a Comment

0 Comments