https://monetag.com/?ref_id=TTIb Washindi wa mbio za Rock city Marathon watembelea Kisiwa cha saa nane | Muungwana BLOG

Washindi wa mbio za Rock city Marathon watembelea Kisiwa cha saa nane


Na Maridhia Ngemela,Mwanza.

 Wananchi wametakiwa kuweka utaratibu mzuri wa kufanya mazoezi ili kuimalisha afya zao ikiwa ni njia moja wapo ya kuwa imara kiafya ,kiakili na utendaji kazi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Utalii Mary Masanja wakati akizungumza katika mashindano ya mbio za rock city marathon msimu wa 12 yaliyofanyika Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza. 

 Masanja  amewapongeza waandaji  wa mbio hizo  Capital Plus International kwa kuweka utaratibu mzuri kwa washiriki wa Rika zote ambapo zaidi ya washiriki 2000 waliweza kushiriki katika mbio hizo ikiwa ni njia moja wapo ya kufanya mazoezi na kujipatia kipato kupitia mchezo huo kwakuwa tumepata washindi katika zoezi hili Mimi kama naibu Waziri wa utalii nawapa nafasi ya kwenda kutembelea kisiwa cha saa nane ili kuendelea kutangaza utalii wa ndani na nawasisitiza washiriki mliopo hapa na wananchi kwa ujumla siku za mapumziko mpange ratiba vizuri muwe mnakwenda kutembelea mbuga za wanyama ,vivutio mbalimbali mkajifunze pia na kuna nafasi nzuri za kukaa mnafanya maongezi ya familia.

"Naomba muendelea kushirikiana kwa kipindi kingine ili kuweza kufanikisha mashindano hayo kwani yamewakutanisha na watu mbalimbali na pia mnaweza kupata wateja wapya ambao wanatamani kushiriki zoezi hili kwa msimu ujao amesema Masanja

Amesema kupitia mashindano hayo kuna hamasisha utalii kwani utalii ni sekta mtambuka ambayo inamuwezesha mwananchi kukuza uchumi na kupata wageni kutoka sehemu mbalimbali.

"Tutaendelea kushirikiana kwenye mashindano mbalimbali maana tunaamini kupitia mbio hizi utalii utakuwa na mwananchi atafaidika na uchimi wa nchi utakuwa.

Aliongeza kuwa Oktoba 30 mwaka huu kutakuwa na Buligi chato marathon itakayofanyika mkoani Geita ni vema washiriki kushiriki katika mashindano hayo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amewasisitiza wananchi wa Wilaya hiyo kuendelea na utaratibu wao wa kufanya mazoezi ambao unalengo la kuimalisha afya ili kuepukana na maradhi mbalimbali. Ikiwemo uviko 

Miongoni mwa washiriki wa mbio hizo Jafeph deuson ameshiriki mbio za kilometa 21 ambapo ameshika nafasi ya kwanza amewashauri vijana kuweka utaratibu wa kuwa wananshiriki mchezo huo wa mbio kwani ni mchezo ambao unajenga afya ,akili na unakuwezesha kuwa na nidhamu ikiwa ni njia moja wapo ya kujipatia kipato.

Jesca Tito ameshiriki mbio za kilomita tano alipata nafasi ya kutembelea kisiwa cha saa nane kutokana na kupata ushindi katika mbio hizo amewaomba Watanzania kutembelea mbuga mbalimbali ikiwa ni njia moja wapo ya kukuza uchumi wa Nchi.

 Kwa upande wake Eva Malya Kamishina Msaidizi mkuu wa hifadhi ya Taifa kisiwa cha saa nane   amesema kuwa kisiwa  hicho kina vivutio mbalimbali ikiwemo swala,tumbili,Simba,tausi na nyumbu.

Malya amesema kuwa,wakazi wa Mwanza jitokezeni kwa wingi ili mjifunze mambo mbalimbali na watoto pia mje nao ili waone wanyama siyo kusoma kwenye vitabu tuu.

 

Post a Comment

0 Comments